Lugha Nyingine
China yaonesha kwa umma kwa mara ya kwanza vazi la wanaanga wakati wa kutua mwezini
Picha hii ikionyesha vazi la wanaanga wa China wakati wa kutua mwezini lililotangazwa na Shirika la Anga ya Juu la China. (Xinhua) |
CHONGQING - Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) siku ya Jumamosi lilionesha kwa umma vazi la wanaanga wakati wa kutua mwezini, likichukua maoni kutoka kwa umma kupewa jina lake.
Likionyeshwa kwenye Baraza la tatu la Teknolojia za Vazi la Suti ya Anga ya Juu lililoandaliwa na Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Wanaanga cha China katika Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China, vazi hilo jeupe limepambwa kwa michirizi mwekundu.
Michirizi hiyo mwekundu kwenye sehemu ya juu ya mwili imetokana na riboni kutoka kwa Sanaa maarufu ya "Apsara wanaoruka" (flying apsaras) ya Dunhuang, wakati ile iliyo sehemu ya chini ya mwili inafanana na mwanga wa kurusha roketi.
Kwa mujibu wa video iliyotolewa na CMSA, vazi hilo limetengenezwa kwa nyenzo za kinga ambazo zinaweza kukinga vyema wanaanga dhidi ya mazingira ya joto na vumbi la mwezini. Lina vifaa vya paneli ya udhibiti jumuishi wenye ufanisi mbalimbali ambavyo ni rahisi kufanya kazi, pamoja na kamera za kurekodi matukio ya karibu na ya umbali mrefu.
Vazi hilo lina glavu zinazonyumbulika na za uhakika, kofia ngumu ya kujikinga kichwani ya kipanorama, na viungio vilivyorekebishwa kwa mazingira ya kani ya chini. Muundo wa jumla wa vazi hilo ni wa mwepesi, ambao ni mwafaka kwa kufanya kazi kwenye mwezini.
Kwa mujibu wa Li Meng kutoka Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Wanaanga cha China, uundaji wa vazi hilo ulianza Mwaka 2020, ukilenga kutengeneza suti ya mwezini ambayo ni nyepesi, imara, ya kutegemeka na salama. Uundaji wake umepata mafanikio mengi muhimu ya kiteknolojia.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma