Lugha Nyingine
Tazama! Teknolojia za hali ya juu kwenye "Gati la Kupendeza"
Picha ikionyesha Gati la Bandari ya Tianjin, China likiwa na pilika nyingi. (Picha kwa hisani ya Bandari ya Tianjin) |
Katika majira ya mpukutiko kwenye kando za ghuba ya Bahari Bohai, kreni za kupakia na kupakua mzigo, kreni kwenye bandari na makontena kwenye gati la Bandari ya Tianjin, Kaskazini mwa China ni yenye rangi mbalimbali ya kupendeza. Hili ni Gati la Pili la Makontena la Kampuni ya Bandari ya Tianjin, ambalo ni gati la kwanza duniani la "teknolojia za kisasa za kutoa kaboni sifuri".
Kreni za rangi mbalimbali za kupakia na kupakua mzigo kwenye bandari zenye usanifu kipekee wa uzuri wa kiviwanda zimelipatia gati hilo jina la "Gati la Kupendeza la Rangi Mbalimbali".
Gati hilo ni la kiwango cha juu zaidi cha bandari duniani katika mchakato kamili wa kiotomatiki na ushughulikiaji wa kisasa wa makontena. Tofauti na kazi za magati mengine yenye michakato kamili ya kiotomatiki, Bandari ya Tianjin imekuwa ya kwanza kuanzisha ujumuishaji na utumiaji wa teknolojia kadhaa za hali ya juu zikiwa na haki miliki za ubunifu za China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma