Lugha Nyingine
Tamasha lafanyika kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China
Tamasha likifanyika Beijing kusherehekea maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China (PRC), Septemba 29, 2024. (Xinhua/Ju Peng)
BEIJING - Tamasha la muziki limefanyika katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing usiku wa kuamkia leo Jumatatu kusherehekea maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, ambapo Rais Xi Jinping wa China, viongozi wengine wa Chama na serikali wakiwemo Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng, pamoja na viongozi waandamizi wastaafu walikuwa miongoni mwa zaidi ya watu 3,000 walioshiriki kwenye tamasha hilo.
Tamasha hilo lilijumuisha muziki wa okestra, uimbaji wa kwaya, upigaji wa ala za jadi, na piano, upigaji muziki wa bendi, na maonyesho mengine ya michezo ya Sanaa. Limemalizika kwa uimbaji wa watu wote wa wimbo uitwao "Taifa Letu". Siku ya Taifa ya China ni Tarehe Mosi, Oktoba kila mwaka.?
Tamasha la muziki likifanyika Beijing kusherehekea maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, Septemba 29, 2024. (Xinhua/Ju Peng)
Tamasha la muziki likifanyika Beijing kusherehekea maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China Septemba 29, 2024. (Xinhua/Ju Peng)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma