Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atunuku nishani za taifa na hadhi za heshima za kitaifa za China
Xi Jinping akiingia kwenye ukumbi wa hafla ya kukabidhi nishani za taifa na hadhi za heshima za kitaifa za Jamhuri ya Watu wa China pamoja na wapokeaji kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 29, 2024. (Xinhua/Yan Yan) |
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping leo Jumapili amewakabidhi nishani watunukiwa nishani za taifa na hadhi za heshima za kitaifa, ambazo ni heshima za juu kabisa za serikali ya China, kabla ya maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.
Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametoa heshima hizo za juu kabisa za taifa kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing.
Askari mstaafu shujaa wa vita Huang Zongde, ambaye ametunukiwa nishani ya taifa, na Dilma Rousseff, Mkuu wa Benki Mpya ya Maendeleo na rais wa zamani wa Brazil, aliyepokea nishani ya Urafiki, wamezungumza kwenye hafla hiyo.
Watu 15 wametunukiwa nishani hizo za kitaifa na hadhi za heshima.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma