Lugha Nyingine
Sudan yasema FOCAC ni jukwaa muhimu kwa China na Afrika kufanya ushirikiano
Waziri wa Nishati na Petroli wa Sudan Dkt. Mohieddin Naeem Mohamed Saeed amesema, ukweli umethibitisha kuwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) limehimiza utekelezaji wa miradi mingi muhimu ya miundombinu barani Afrika.
Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano na Shirika la Habari la Xinhua katika mji wa Bandari ya Sudan, Bw. Saeed amesema kwa miaka mingi, China na Sudan zimekuwa na ushirikiano wenye manufaa katika sekta nyingi ikiwemo sekta ya mafuta, na tangu miaka ya 1990, kwa msaada wa China, Sudan imeanzisha mnyororo kamili wa sekta ya mafuta na kubadilishwa kutoka nchi inayoagiza mafuta hadi nchi inayosafirisha mafuta.
Pia amesema, Sudan inatarajia kuanzisha ushirikiano na China katika sekta ya uzalishaji wa umeme, na inakaribisha kampuni za China kuwekeza nchini Sudan ili kuendeleza urafiki mkubwa kati ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma